UCHUMI WA KUTISHA
Wahenga walisema mnyonge mnyongeni haya ndio Masaibu yanayo wapata Wakenya kutokana na mfumuko wa bei za bidhaa nchini huku serikali yake ikijitia hamnazo na kuto wajali raia wake.
![]() |
| HISANI google |
Taifa la Kenya ni taifa lenye uchumi Bora zaidi Afrika mashariki. Kenya Ina uchumi wa takriban trillioni Kumi na tatu lakini ni jambo la kuhuzunisha kuona kwamba licha ya uchumi wa mamilioni ya pesa wananchi wa taifa hili wanaishi maisha ya umasikini uliomithilika wananchi Hawa wanalala njaa Kwa kushindwa kumudu gharama ya maisha. Mfumuko wa wa bei ya bidhaa hivi majuzi nchini umewaacha wananchi katika njia panda huku familia kadhaa zikishindwa kabisa kukidhi hitaji la lishe Bora kila siku.
| Picha hisani |
Bei ya bidhaa nchini imepanda maradufu,huku nalo taifa likijiandaa Kwa uchaguzi mkuu Agosti Tisa. Wananchi wapiga kura wanaonekana kukerwa sana na bei za bidhaa.Maisha yamezidi kuwa magumu nchini huku wananchi wakiishi Kwa kubahatisha na kulia silele mama.
Licha ya uchochole na umasikini gharama ya maisha nayo inatishia wakadamiza zaidi kuwapotezea mbali.Imekuwa muhali Kwa jamii nyinyi nchini kupata lishe tupilia mbali lishe Bora. Taifa liko na ukame wa mvua na wananchi nao pia wakilalimikia ukame wa pesa,licha ya taifa kuwa na uchumi mkubwa ni dhahiri sharing kuwa hakuna mtiririko wa pesa kuwafikia masikini,pesa zinabakia mifukoni mwa wakubwa,viongozi,mabwenyenye na wachache jambo ambalo limechangia kuwafanya wakenya wengi masikini na kushindwa kukidhi mahitaji msingi.Wakenya wengi hawana kazi na wale waliofanikiwa kupata kazi za sulubu nayo mishahara inabakia kuwa ya sulubu.Wachuuzi wadogo wamefunga biashara za baada Yao kuonana hasara isiyokadirika kutoka na kupandishwa Kwa bei ya bidhaa maalum.
Ombi langu Kwa mtukufu raise,ingawa najua kazi Yako umeimaliza na Sasa ni wakati wako wa kwenda mapumzikoni,ningeomba ufanye jambo moja la busara na ambalo pia naona litaacha jina lako katika kumbukumbu yetu ya viongozi Bora kama rais na kiongozi aliyejali na kuweka mahitaji ya wananchi wake.Ninakuomba na Wakenya wote rais tunaomba kabla Yako kumaliza hatamu Yako uziangazie bei za bidhaa nchini na kuzishukisha na kuacha bei ya bidhaa ikiwa pale ulipoipata miaka Tisa iliyopita ulipoingia uongozi mwaka 2013!!
Je inawezekana?




Bei ya bidhaa tishio kwa sasa
ReplyDeleteViongozi tunao wachagua ndo wanafaa kututetea lakini kama kisu ndo hakimu kwa kesi ya kuku
ReplyDeleteHii kenya tunahamaa
ReplyDeleteHali zenyewe ngumu sana
ReplyDeleteMafuta in gold manzeee...
ReplyDeleteKazi nzuri👌🏾
ReplyDeleteKuntu! Tunataka Kenya nyingine lakini😂😂
ReplyDeleteTuhame tu Kenya
ReplyDelete