UCHUMI WA KUTISHA
Wahenga walisema mnyonge mnyongeni haya ndio Masaibu yanayo wapata Wakenya kutokana na mfumuko wa bei za bidhaa nchini huku serikali yake ikijitia hamnazo na kuto wajali raia wake. HISANI google Taifa la Kenya ni taifa lenye uchumi Bora zaidi Afrika mashariki. Kenya Ina uchumi wa takriban trillioni Kumi na tatu lakini ni jambo la kuhuzunisha kuona kwamba licha ya uchumi wa mamilioni ya pesa wananchi wa taifa hili wanaishi maisha ya umasikini uliomithilika wananchi Hawa wanalala njaa Kwa kushindwa kumudu gharama ya maisha. Mfumuko wa wa bei ya bidhaa hivi majuzi nchini umewaacha wananchi katika njia panda huku familia kadhaa zikishindwa kabisa kukidhi hitaji la lishe Bora kila siku. Picha hisani Bei ya bidhaa nchini imepanda maradufu,huku nalo taifa likijiandaa Kwa uchaguzi mkuu Agosti Tisa. Wananchi wapiga kura wanaonekana kukerwa sana na bei za bidhaa.Maisha yamezidi kuwa magumu nchini huku wananchi wakiishi Kwa kubahatisha na kulia silele mama. Licha ya uchochole na ...